| Sea View/ City View Studio Room | Jisikie uko nyumbani katika chumba cha kisasa chenye utulivu katika Jiji lenye shughuli nyingi la Dar es Salaam cha mita za mraba 43 aina ya Studio Room, ambacho ni kikubwa kimtindo na kinafasi. Kinafaa kwa wageni wa kibiashara au starehe, mahali hapa pa faragha panapoburudisha panajumuisha kitanda aina ya king, jiko, samani na visitawishi vya kisasa na madirisha yanayoanzia sakafuni hadi darini yanayoonyesha mandhari nzuri ya jiji na bandari. |
| |
|
| Sea View/ City View One Bedroom Apartment | Ingia katika sehemu yako ya faragha Jijini ukiwa Johari Rotana. Chumba chetu Kimoja cha Kupanga kikiwa katika mtindo wa kisasa, kinafaa kwa wageni wanaokaa kwa muda mrefu. Chenye ukubwa wa mita za mraba 87, kinajumuisha kitanda aina ya king, samani za kisasa, jiko, meza ya kufanyia kazi na nafasi kubwa zaidi kwa ajili ya kazi au kupumzika baada ya kumaliza siku yenye shughuli nyingi. Furahia starehe ya mandhari nzuri ya anga la jiji na bandari kupitia madirisha yanayoanzia kwenye sakafu hadi darini ambayo yanaingiza nuru ndani ya chumba chako na mwanga wa kifahari wa jua la Dar es Salaam wakati wa mchana na taa za jiji wakati wa usiku. |
| |
|
| Sea View / City View Two Bedroom Apartment | Jisikie nyumbani katika ghorofa yetu ya kisasa yenye vyumba viwili vya kulala, iliyowekewa samani zote, katikati ya jiji la Dar es Salaam. Inafaa kwa familia au makundi ya watu, ghorofa hii ya mita za mraba 130 ina vitanda viwili vya ukubwa wa King katika vyumba tofauti, jikoni zilizo na vifaa vyote muhimu, samani za kisasa, na nafasi ya kutosha pamoja na mandhari ya kuvutia ya bahari au jiji – kwa kweli utajisikia kama uko nyumbani. |
| |
|
|
|