Iwe unakwenda Dar es Salaam kwa ajili ya biashara au starehe, Johari Rotana inakupa ufahari na urahisi katika eneo pendwa la kibiashara Katikati ya Jiji karibu na bandari, Reli Kuu na eneo la kiuchumi la Jiji. Hoteli pia ipo karibu na vivutio maarufu vya utalii na maeneo ya kihistoria jijini ikiwa ni pamoja na Makumbusho ya Taifa , Makumbusho ya Vijiji, Kanisa Kuu la Mt. Yosefu, Bustani za Mimea, maduka mengi, migahawa na masoko ambayo yote yapo ndani ya umbali wa kutembea kwa mguu. Iliopo katika Mtaa wa Sokoine, upande wa pili wa Ferry ya Zanzibar, pembezoni ya bandari na upwa, jengo la hoteli ni sehemu ya MNF Square lenye matumizi mchanganyiko pamoja na maduka ya rejareja, maeneo ya ofisi na maegesho ya magari, wakati sehemu za kisasa za kupata huduma kwa urahisi ikiwa ni pamoja na benki, hospitali na mitandao ya usafiri yote yapo ndani ya umbali wa kutembea kwa mguu. Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere upo umbali wa dakika 30 tu kwa gari, umbali sawa na wa kwenda katika Hifadhi nzuri ya Baharini ya Kisiwa cha Bongoyo kusini mwa Pwani ya Tanzania, mahali palipo na fukwe nyingi, visiwa vya kupendeza sana na maeneo mazuri ya kuogelea na kupiga mbizi. Kwa wageni wanaosafiri kwa gari kwa kutumia mfumo wa kuongoza wa GPS, eneo la hoteli ni: Latitudo: -6.819809635 / Longitudo: 39.286862310. Johari Rotana pia hutoa sehemu ya maegesho ya magari kwa wageni. |